Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

Christian Bella asema sababu akatunga 'Nani Kama Mama'

 
Mwimbaji wa dansi, Christian Bella ameeleza kuwa alimshuhudia mkewe akijifungua, kitu kilichomfanya aandike wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz. Christian Bella ambaye ni kiongozi wa Malaika Band ameeleza hayo wakati akiongea na gazeti la Mwanaspoti.
“Mwaka 2012 nilienda Sweden kwa mke wangu ambaye alikuwa anajifungua hivyo nililazimika kuwepo ili kushuhudia mtoto wangu akizaliwa .Nilishuhudia kila kitu na sasa nina watoto wawili wa kiume Jordan (7) na Hance (2).” Amesema Christian Bella.
“Niliamua kutunga wimbo huu baada ya kushuhudia hatua zote mke wangu alipojifungua, kiukweli mwanamke anatakiwa kuheshimika tofauti na wanavyowachukulia, hapo ndipo niliona kuna haja ya kuimba wimbo wenye ujumbe huu.”

Shilole kuwania ubunge wa Igunga


Inawezekana kabisa Shilole akawa msanii ambaye ungedhani angewekeza zaidi kwenye duka la urembo, nguo ama hata madini kwa jicho la kawaida kama akitaka kufanya biashara mbali na muziki. Lakini kwa jicho la tatu usimchukulie hivyo.

Msanii huyo ambaye ni mzaliwa wa Igunga  panapofahamika zaidi kama kwa Rostam Aziz, mbunge aliyekaa muda mrefu madarakani kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Kafumu ambaye ni mbunge wa sasa, amepanga kuingia kwenye mchakato wa ubunge kwa lengo la kulitwaa jimbo hilo.
Shilole aliiambia Bongo Dot Home kuwa amefanya uamuzi wa kugombea katika jimbo hilo kwa kuwa anaona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa na yeye kama mzawa anaamini anaweza kuwasaidia zaidi wananchi wa Igunga.
“Ni kwa sababu ya matatizo yaliyopo. Nimekuwa nikienda naona matatizo kila siku yapo..ndio maana naona kama naweza kusimama na watu wengi sana wakanisikiliza kwa nini nisijitokeze kuwasaidia matatizo yao. Nimezaliwa pale mimi, nakijua kitongoji kimoja baadaya kingine.” Ameeleza.
“Nikipata ubunge kwanza kabisa nitadeal na akina mama, wafanyabiashara ndogondogo waweze kujikwamua vizuri. Pili vijana waweze kupata ajira kwa sababu sasa hivi naona vijana wa Igunga ajira zimekuwa ngumu kupatikana. Kuweka vitendea kazi ambavyo vitakuwa rahisi sana kuweza kufanya kazi na kutoa vijijini kupeleka mjini.” Alijinadi Shilole.
Akiwa kwenye kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm, mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na muziki yeye ni mkulima wa mpunga na ana mashamba mengi ya mpunga huko Igunga.

Monday, August 4, 2014

Collabo ya Davido na Drake hii hapa..


Msanii wa Nigeria, Davido anaendelea kusaka nafasi ya kuwa kati ya wasanii wakubwa zaidi sio tu Afrika bali dunia nzima kwa ujumla.
Siku kadhaa baada ya kutangaza collabo na Meek Mill na Rick Ross, mwimbaji huyo wa ‘Aye’ ameiambia Encomium kuwa yuko katika mazungumzo na rapper wa Young Money, Drake kwa ajili ya kufanya collabo kwa usimamizi wa Don Jazzy.
“I might not call it ‘dream collaboration’ but by His grace, it’ll work, and already, I am talking with Drake and Don Jazzy. We would work on something very unique.” Amesema Davido.
Amefafanua kuwa mpango wake wa kufanya collabo na wasanii wakubwa wa kimataifa au hata wadogo sio kwa lengo la kusaka umaarufu.
“My collaboration with other artistes is not a ploy to be popular, after all, I am not going to take the glory alone. Apart from the artistes you collaborated with, you never know what song can make you big as well. It doesn’t matter if you feature a big or up-and-coming artiste. That’s the main reason I am doing this.”

Maneno ya Ay baada ya kufika Ikulu Marekani na alichokutana nacho

A.Y tayari ameshafika Marekani na wameanza kwa kukutana na Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval.


Huu msafara wa wasanii kutoka Africa unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y ambapo kesho wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama.


Baada tu ya kufika, Ay kaniambia kitu cha tofauti alichokutana nacho kwenye Ikulu hii ni kwamba jamaa wanakwenda na dress code kutokana na siku, yani imepangwa kuna mavazi ya kuvaa kutokana na siku… kwa weekend ambayo Ay na wenzake waliitembelea Ikulu mtu yeyote haruhusiwi kuvaa suti hivyo utawakuta Wafanyakazi wengine na kaptula au jeans.
Hata kina Ay wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend.

Ay anasema kingine ni kwamba Obama kila wiki anatenga siku ya kukutana na Watoto kutoka sehemu mbalimbali wanaotembelea Ikulu.

 
Blogger Templates