Inawezekana uliwahi waona kwenye matamasha mbalimbali Wema Sepetu na
Diamond wakiwa pamoja lakini hua inakua kama ‘Sapraiz’ ili pengine
kuleta hamasa kwa mashabiki wao,sasa rasmi hii ni show ya kwanza ambayo
itamueka Diamond Platnumz na Wema Sepetu kwenye jukwaa moja.
Wakazi wa Mtwara wamepata zali hili la kuona mastar hawa wakiwa
wanaupeleka usiku wa Hills and Tie ambao umedhaminiwa na kampuni ya simu
za mkononi ya Vodacom,Meneja Masoko wa Vodacon Kelvin Twissa amesema
huu utakua mkoa wa Kwanza na kama Mtwara watatoa sapoti wanategemea
kuifanya iwe tour.
Hii ni namba maalum kwa ajili ya wateja wa vodacom kuweza kununua
tiketi kupitia M pesa kwa simu zao za mkononi ambapo kwa yeyote
atakaenunua atapata punguzo la asilimia 20 namba hiyo ni 0754 980 769.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments:
Post a Comment