Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, April 14, 2014

BREAKING NEWS:bomu lililolipuka Arusha April 13 usiku, idadi ya waliojeruhiwa.


Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.

Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.

0 comments:

 
Blogger Templates