Wimbo
huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka katika mahadhi tofauti tofauti
ya muziki wa hapa Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na
muziki wa injili.
Inawezekana
ikawa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,wasanii 50 tofauti
kuimba wimbo kwa pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa
wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.
Miongoni mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni pamoja na
Kadjanito,Mwasiti,Linah,Christina Shusho,Khadija Kopa,Frola Mbasha,Ommy
Dimpoz,Diamond,Josse Mara,Kalala Jr,Ali Kiba,Peter Msechu,Mrisho
Mpoto,Abdul Kiba,Mzee Yusuph,Angel,Mwana Fa,Nikki Wa pili,G Nako,God
Zilla,Madee,Asley,Shaa,Mandojo,Domokaya,Shilole na Roma Mkatoliki.
0 comments:
Post a Comment