Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

FILAMU

  Baadhi  ya aina maarufu za Filamu Duniani

     Kwa kuzingatia maudhui ya filamu husika kumetokea kuwepo kwa aina kadhaa ya filamu
katika 'industry' kubwa za filamu duniani kama Hollywood na Bollywood..na kufanya wapenzi wa filamu duniani kuendelea kuvutiwa zaidi na kuzitazama kwa wingi filamu hizo
Baadhi ya aina izi kwa kifupi na kama zifuatazo:

DRAMA

Aina hii ya filamu hubeba maudhui yanayohusu visa na matatizo yanayotokea katika
familia zetu.Filamu hizi huelezea sana matatizo yanayohusiana na mambo ya ajira,kipato,
huduma za kila siku kwa watoto na mke,ulevi,usaliti,matumizi ya madawa ya kulevya na bangi,na
mengineyo mengi namna yanavyosababisha kuyumba kwa familia na ndoa.Mfano wa filamu hizo ni
Good Deeds,Pursuit of happiness,A good man is hard to find na Seven pound.

COMEDY

Hii hujumuisha filamu zote zenye visa na matukio ya ucheshi.Filamu hizi huelezea namna watu
wanapochukulia vitu kwa upande mwingine na kupelekea kufanya uzembe au kutoa kauli zinazopelekea kuwa kichekesho
kwa hadhira husika.
Pia filamu hizi mara nyingi hazina maudhui ya kupelekea hisia kali kwa hadhira kama masikitiko na huruma.
Mfano wa filamu hizo ni 21 Jump street,White chicks,Dance Freak,American pie,Dectactor na Mr.Bones

ACTION

Visa vinavyopelekea mapigano aidha ya mwili,silaha za moto,mishale,mikuki an nyinginezo ndiyo
huwepo katika filamu za aina hii.Filamu za namna hii zimeonekana kuchukua hadhira kubwa duniani
kutokana na kuhusisha burudani ya mapigano yenye msisimko mkubwa.
Pia filamu hizi hutengenezwa kwa bajeti kubwa kutokana na uharibifu wa majengo na vyombo vya usafiri
wakati wa upiganaji.
Mfano wa filamu hizo ni Die Hard,Commando,Hard Tagert,Enter the dragon,Romeo must die na War bus.

SUSPENSE

Hujumuisha mitiririko wa matukio ya kikatili kati ya watu na watu,watu na wanyama au wanyama na wanyama.
Filamu hizi huwa na matukio ya visasi,hupungufu wa akili na vyanzo vingine vinavyopelekea ukatili kwa
wahusika na mara nyingine hata watu wasio na hatia,
Mfano wa filamu hizo ni Hostel,SAW na Final destinatination.

HORROR

Huwa na mtiririko wa matukio ya kutisha yanayohusiana na mambo ya kiroho kama mizimu,mapepo na uchawi.
Mfano Evil  dead,Drag me to Hell,Baracuda,Nightmares in Elm street,Messenger an Mama.

SCIENCE FICTION

Huwa na matukio mengi yasiyo husiana na matukio ya kweli ya kila siku.Visa vyake huwa ni vya kufikirika na huwa
si vya kweli.
Pia vyanzo vyake huhusisha mambo ya kisayansi mfani kibailojia,kifizikia,kikemia ili kuleta chanzo chenye maana.
Mfano wa filamu hizo ni I am number Four,Avengers,Star trek,Spiderman,X-Men,John carter na Starship Troopers.

LOVE STORY AND ROMANCY

Hizi ni zile filamu zenye hadithi za mahaba na mapenzi baina ya mwanaume na mwanamke,mwanaume na mwanaume
au mwanamke na mwanamke.
Huwa na visa vya kusikitisha,kusisimua,kuburudisha na kufundisha.Pia huelezea uwepo wa matatizo katika mapenzi,
kuwa na mahusiano ambayo si sahihi,kuvunjwa mioyo na usaliti.
Mfano wa filamu hizo ni Friends of Benefits,Mboni yangu,Kal ho na hoo,kuch kuch hota hai na Flower.

ADVENTURE

Ni filamu zinazo onesha wahusika kuwa na safari fulani kufuata kitu fulani cha siri na thamani kilichogunduliwa
mfano mlima wenye dhahabu,maandiko ya siri,Kito cha thamani na mtu muhimu.Safari hiyo ndiyo hubeba visa
vyote hadi mwisho wa safari.
Mfano wa filamu hizo ni Hobbit,Lord of the ring,Legend of the seeker,Pirates of Carribean na OZ World.

FANTASY AND THRILL

Huwa na muhusika mmoja ambaye anaokoa jamii fulani bila kutambulika na jamii husika.Mhusika huwa na uwezo
mkubwa na wa tofauti bila kueleweka chanzo sahihi cha uwezo huo.
Mfano filamu hizo ni Spiderman,Batman na Hulk.

FACTIAL ,MYSTERY& CRIME

Hizi ni filamu zinazoelezea sana mantiki na visa vya kutumia akili sana.
Pia huhusisha uharifu na chanzo cha kutatanisha cha uharifu huo.Mtiririko wa kutafuta majibu na visababishi au vyanzo
vya matukio fulani ya uharifu huunda filamu husika.
Mfano wake ni Unknown,Enemy of the state,The tourist na The exam.

ANIMATION

Hizi ni filamu zinazotengenezwa kwa nia ya kuburudisha na wahusika wake huwa si watu alisia bali hutengenezwa kwenye kompyuta na kuwekewa uhai wa vitendo na mazungumzo yaani 'animated characters'.
Mfano wake ni Megamind,Rio,Tangled,Bolt and Turbo

Hizo ni baadhi ya aina mbalimbali kubwa ya filamu duniani.kwa maoni na maswali wasiliana nasi
kwa
E-Mail:newdayprotanzania@gmail.com
          

0 comments:

 
Blogger Templates