Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

Shilole kuwania ubunge wa Igunga


Inawezekana kabisa Shilole akawa msanii ambaye ungedhani angewekeza zaidi kwenye duka la urembo, nguo ama hata madini kwa jicho la kawaida kama akitaka kufanya biashara mbali na muziki. Lakini kwa jicho la tatu usimchukulie hivyo.

Msanii huyo ambaye ni mzaliwa wa Igunga  panapofahamika zaidi kama kwa Rostam Aziz, mbunge aliyekaa muda mrefu madarakani kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Kafumu ambaye ni mbunge wa sasa, amepanga kuingia kwenye mchakato wa ubunge kwa lengo la kulitwaa jimbo hilo.
Shilole aliiambia Bongo Dot Home kuwa amefanya uamuzi wa kugombea katika jimbo hilo kwa kuwa anaona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa na yeye kama mzawa anaamini anaweza kuwasaidia zaidi wananchi wa Igunga.
“Ni kwa sababu ya matatizo yaliyopo. Nimekuwa nikienda naona matatizo kila siku yapo..ndio maana naona kama naweza kusimama na watu wengi sana wakanisikiliza kwa nini nisijitokeze kuwasaidia matatizo yao. Nimezaliwa pale mimi, nakijua kitongoji kimoja baadaya kingine.” Ameeleza.
“Nikipata ubunge kwanza kabisa nitadeal na akina mama, wafanyabiashara ndogondogo waweze kujikwamua vizuri. Pili vijana waweze kupata ajira kwa sababu sasa hivi naona vijana wa Igunga ajira zimekuwa ngumu kupatikana. Kuweka vitendea kazi ambavyo vitakuwa rahisi sana kuweza kufanya kazi na kutoa vijijini kupeleka mjini.” Alijinadi Shilole.
Akiwa kwenye kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm, mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na muziki yeye ni mkulima wa mpunga na ana mashamba mengi ya mpunga huko Igunga.

0 comments:

 
Blogger Templates