A.Y tayari ameshafika Marekani na wameanza kwa kukutana na
Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii
wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White
House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval.
Huu msafara wa wasanii kutoka Africa unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa
Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y
ambapo kesho wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama.
Baada tu ya kufika, Ay kaniambia kitu cha tofauti alichokutana nacho
kwenye Ikulu hii ni kwamba jamaa wanakwenda na dress code kutokana na
siku, yani imepangwa kuna mavazi ya kuvaa kutokana na siku… kwa weekend
ambayo Ay na wenzake waliitembelea Ikulu mtu yeyote haruhusiwi kuvaa
suti hivyo utawakuta Wafanyakazi wengine na kaptula au jeans.
Hata kina Ay wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend.
Ay anasema kingine ni kwamba Obama kila wiki anatenga siku ya kukutana na Watoto kutoka sehemu mbalimbali wanaotembelea Ikulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment