Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Featured Posts

Tuesday, August 5, 2014

Christian Bella asema sababu akatunga 'Nani Kama Mama'

 
Mwimbaji wa dansi, Christian Bella ameeleza kuwa alimshuhudia mkewe akijifungua, kitu kilichomfanya aandike wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz. Christian Bella ambaye ni kiongozi wa Malaika Band ameeleza hayo wakati akiongea na gazeti la Mwanaspoti.
“Mwaka 2012 nilienda Sweden kwa mke wangu ambaye alikuwa anajifungua hivyo nililazimika kuwepo ili kushuhudia mtoto wangu akizaliwa .Nilishuhudia kila kitu na sasa nina watoto wawili wa kiume Jordan (7) na Hance (2).” Amesema Christian Bella.
“Niliamua kutunga wimbo huu baada ya kushuhudia hatua zote mke wangu alipojifungua, kiukweli mwanamke anatakiwa kuheshimika tofauti na wanavyowachukulia, hapo ndipo niliona kuna haja ya kuimba wimbo wenye ujumbe huu.”

Shilole kuwania ubunge wa Igunga


Inawezekana kabisa Shilole akawa msanii ambaye ungedhani angewekeza zaidi kwenye duka la urembo, nguo ama hata madini kwa jicho la kawaida kama akitaka kufanya biashara mbali na muziki. Lakini kwa jicho la tatu usimchukulie hivyo.

Msanii huyo ambaye ni mzaliwa wa Igunga  panapofahamika zaidi kama kwa Rostam Aziz, mbunge aliyekaa muda mrefu madarakani kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Kafumu ambaye ni mbunge wa sasa, amepanga kuingia kwenye mchakato wa ubunge kwa lengo la kulitwaa jimbo hilo.
Shilole aliiambia Bongo Dot Home kuwa amefanya uamuzi wa kugombea katika jimbo hilo kwa kuwa anaona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa na yeye kama mzawa anaamini anaweza kuwasaidia zaidi wananchi wa Igunga.
“Ni kwa sababu ya matatizo yaliyopo. Nimekuwa nikienda naona matatizo kila siku yapo..ndio maana naona kama naweza kusimama na watu wengi sana wakanisikiliza kwa nini nisijitokeze kuwasaidia matatizo yao. Nimezaliwa pale mimi, nakijua kitongoji kimoja baadaya kingine.” Ameeleza.
“Nikipata ubunge kwanza kabisa nitadeal na akina mama, wafanyabiashara ndogondogo waweze kujikwamua vizuri. Pili vijana waweze kupata ajira kwa sababu sasa hivi naona vijana wa Igunga ajira zimekuwa ngumu kupatikana. Kuweka vitendea kazi ambavyo vitakuwa rahisi sana kuweza kufanya kazi na kutoa vijijini kupeleka mjini.” Alijinadi Shilole.
Akiwa kwenye kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm, mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na muziki yeye ni mkulima wa mpunga na ana mashamba mengi ya mpunga huko Igunga.

Monday, August 4, 2014

Collabo ya Davido na Drake hii hapa..


Msanii wa Nigeria, Davido anaendelea kusaka nafasi ya kuwa kati ya wasanii wakubwa zaidi sio tu Afrika bali dunia nzima kwa ujumla.
Siku kadhaa baada ya kutangaza collabo na Meek Mill na Rick Ross, mwimbaji huyo wa ‘Aye’ ameiambia Encomium kuwa yuko katika mazungumzo na rapper wa Young Money, Drake kwa ajili ya kufanya collabo kwa usimamizi wa Don Jazzy.
“I might not call it ‘dream collaboration’ but by His grace, it’ll work, and already, I am talking with Drake and Don Jazzy. We would work on something very unique.” Amesema Davido.
Amefafanua kuwa mpango wake wa kufanya collabo na wasanii wakubwa wa kimataifa au hata wadogo sio kwa lengo la kusaka umaarufu.
“My collaboration with other artistes is not a ploy to be popular, after all, I am not going to take the glory alone. Apart from the artistes you collaborated with, you never know what song can make you big as well. It doesn’t matter if you feature a big or up-and-coming artiste. That’s the main reason I am doing this.”

Maneno ya Ay baada ya kufika Ikulu Marekani na alichokutana nacho

A.Y tayari ameshafika Marekani na wameanza kwa kukutana na Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval.


Huu msafara wa wasanii kutoka Africa unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y ambapo kesho wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama.


Baada tu ya kufika, Ay kaniambia kitu cha tofauti alichokutana nacho kwenye Ikulu hii ni kwamba jamaa wanakwenda na dress code kutokana na siku, yani imepangwa kuna mavazi ya kuvaa kutokana na siku… kwa weekend ambayo Ay na wenzake waliitembelea Ikulu mtu yeyote haruhusiwi kuvaa suti hivyo utawakuta Wafanyakazi wengine na kaptula au jeans.
Hata kina Ay wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend.

Ay anasema kingine ni kwamba Obama kila wiki anatenga siku ya kukutana na Watoto kutoka sehemu mbalimbali wanaotembelea Ikulu.

Thursday, July 24, 2014

Brand New Song: Country Boy Ft. Blue Mchaka Mchaka


Hii ni ngoma nyingine mpya kutoka kwa Country Boy inaitwa Mchaka Mchaka, ngoma imefanyika chini ya producer Messen Selekta,
Blue ameisimamia vya kutosha chorus ya ngoma hii…
Bonyeza hapa kusikiliza

Tuesday, May 6, 2014

FID Q "NILISTAHILI KUSHINDA TUZO YA KILL, KILA MTU AMEFURAHI BAADA YA KUNIBANIA KWA MUDA MREFU"



Msanii Fid Q amehabarisha kuwa kila mtu amefurahi kwa yeye kushinda Tuzo ya Mwana Hip Hop Bora wa Mwaka , Amesema hiyo inajidhihirisha hata kwenye Social Media kila mtu anasifia na kukubali ishindi wake
                          ..Amasema Amebaniwa Miaka Mingi hiyo tuzo na Hatimae ameipata....

Saturday, May 3, 2014

Hatimaye KTMA 2014 hii hapa, leo usiku


Wahenga wanasema subira yavuta heri. Hilo linathibitishwa, baada ya kusubiri kwa miezi zaidi ya mwili hatimaye leo ndio tuzo kilele cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.


Fuatilia kila tukio live kupitia www.kililager.com/KTMA ukianza na Red Carpet wakati Jokate Mwegelo, Salma Msangi na Millard Ayo wakiwahoji mastaa mbalimbali watakaokuwa wakiwasili katika zuria jekundu na utaweza kujua kina nani wametokezea. Baadae wataungana na Sam Misago wa EATV katika Social Media Lounge ambapo wakuwa wakiwahoji washindi na wateule wengine wa tuzo.

Thursday, May 1, 2014

VIDEO: Sauti sol - Nishike hii hapa

Baada ya skendo nyingi kwa wanamuziki wa kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya, sasa watoka na song jipya kwa jina la "Nishike" kuonesha kuwa

Wednesday, April 30, 2014

Wema Sepetu na Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza rasmi kuwa kwa jukwaa moja

Inawezekana uliwahi waona kwenye matamasha mbalimbali Wema Sepetu na Diamond wakiwa pamoja lakini hua inakua kama ‘Sapraiz’ ili pengine kuleta hamasa kwa mashabiki wao,sasa rasmi hii ni show ya kwanza ambayo itamueka Diamond Platnumz na Wema Sepetu kwenye jukwaa moja.
Wakazi wa Mtwara wamepata zali hili la kuona mastar hawa wakiwa wanaupeleka usiku wa Hills and Tie ambao umedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom,Meneja Masoko wa Vodacon Kelvin Twissa amesema huu utakua mkoa wa Kwanza na kama Mtwara watatoa sapoti wanategemea kuifanya iwe tour. Hii ni namba maalum kwa ajili ya wateja wa vodacom kuweza kununua tiketi kupitia M pesa kwa simu zao za mkononi ambapo kwa yeyote atakaenunua atapata punguzo la asilimia 20 namba hiyo ni 0754 980 769.



Monday, April 28, 2014

WIMBO ULIOWAKUTANISHA WASANII 50 KUTOKA TANZANIA

Wimbo Maalumu wa Muungano ulioimbwa na wasanii 50 kutoka Tanzania ambao kwa pamoja walikaa na kutengeneza wimbo huu,jina la wimbo huu unaitwa Tuulinde umetayarishwa na maproducer wawili Ema the boy na Tuddy Thomas kutoka Soround Sound Studio.


Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki wa hapa Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili.
Inawezekana ikawa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.
Miongoni mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni pamoja na Kadjanito,Mwasiti,Linah,Christina Shusho,Khadija Kopa,Frola Mbasha,Ommy Dimpoz,Diamond,Josse Mara,Kalala Jr,Ali Kiba,Peter Msechu,Mrisho Mpoto,Abdul Kiba,Mzee Yusuph,Angel,Mwana Fa,Nikki Wa pili,G Nako,God Zilla,Madee,Asley,Shaa,Mandojo,Domokaya,Shilole na Roma Mkatoliki.

USIKU WA MKETE FASHION MBEYA

Usiku uliojaa ubunifu na burudani mbalimbali ndani ya ukumbi wa Mtenda Sunset, na kuacha uzoefu  wa kitofauti kwa wakazi wa Mbeya kwani haijawahi tokea fashion show kama hiyo mkoani humo....kama ilivyo pangwa usiku huo ulipambwa na Designer na Models kutoka vyuo vikuu vya Mbeya na pia kutoka Green team photogenic.
Mgeni rasmi,sponsors na waandaaji wa mkete fashion night
Designers na Models wakijiaanda



Na pia wasanii na ma dancers walokuwepo na kuleta radha nyingine poa sana ndani ya usiku wa Mkete fashion.... mashabiki waliburudishwa zaidi na sauti nzuri ya msanii kutoka Mbeya Modolist kwenye usiku huu
Washiriki na wazamini wa fashion show hiyo pia walipewa vyeti vya ushiriki katika usiku wa Mkete





Mkete fashion night ndani ya Mbeya hufanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2014 na kuendelea...
kwa matukio mengine ya like page yetu Extreme Taarifa

Thursday, April 24, 2014

Ni ghafla lakini hii hapa MKETE FASHION NIGHT 2014 Mbeya


Usiku wa Fashion ndani ya ukumbi wa Mtenda hall siku ya jumamosi 26, April,2014 sasa umefika kwa mtu yeyote anakaribishwa katika usiku huu uliojaa fun na  ubunifu kutoka kwa Designers na Models wa Mbeya.. hii sio ya kukosa jamaa
Burudani mbalimbali zaidi ya fashion show zitaletwa kwenyu na vijana wa mbeya na pia wanachuo kutoka Mzumbe,MUST,TIA,CDTI na TEKU ili kuusindikiza usiku huo wa ubunifu..

Tuesday, April 22, 2014

KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P-SQUARE


Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi. 

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.

Thursday, April 17, 2014

TEN HIP HOP FACTS HIZI HAPA

HIP HOP ni aina ya muziki au utamaduni unaopendwa na vijana wengi zaidi duniani na ni aina ya muziki wenye mashabiki wengi zaidi… kuna baadhi ya mambo ambayo najua utakua haufahamu kuhusiana na muziki huu na hujawahi sikia kwa mtu sasa fungua macho nikupe ukweli wa mambo kadhaa..

1.KUNDI LA HIP HOP LA KWANZA LA WANAWAKE
      Tumeona makundi mengi ya hip-hop huwa ni ya wanaume tupu lakini hawa ndio wanawake wa kwanza kuwa pamoja na kutengeneza group moja lililokwenda kwa jina la MARCEDES LADIES

2.KAZI ALIYOFANYA DIDDY KABLA YA KUANZA MUZIKI
     Kwa mara ya kwanza P.diddy alianza kuonekana katika majukwaa ya HIP HOP  akiwa kama “back up” dancer wa Big Daddy Kane.. hapo ndio tunaona kweli everything Start from bottom

3.MARA YA KWANZA JAY Z KU-SHOOT MTU
     Moja kati ya wana hip hop wajasiriamali wenye vitega uchumi vingi nchini Marekani na dunia nzima.. Jigga alianza kupenda pesa akiwa mdogo na hii inaonyesha kuwa Jigga anapenda pesa kuliko utu.. Jigga kachafua biography yake baada ya kum-shoot his blood brother yaani tumbo moja baada ya kumuibia mtonyo tu.

4. PROJECT YA PEKEE ILIYO MPATIA NAS TUNZO YA GRAMMY
     Project ya kwanza naya mwisho ya Nas kunyakua au kubeba tunzo ya grammy… ni ile aliyo muandikia Will Smith nyimbo inaitwa “jiggy with it” Nas hajawahi pata tunzo ya grammy tena tangu project hiyo… Damn Nas!! If I was ur pop ALU DARA I could ask you to stop raping *KIDING*

5.POETIC JUSTICE SEX SCENE
   Kama hujawahiona filamu ya “poetic justice” nakusihi ukaitafute bonge la filamu hilo kuwa na mastaa kibao ndani yake movie hii ilikua ikizungumzia maisha ya mtu mweusi hasa vijana waishio Marekani ndani yake kulikua na Janet Jackson na pia one of the best rapper of all time 2PAC SHAKUR
      Sasa  wakati wa uandaaji wa movie hiyo kuna scene ambayo  2pac na Janet Jackson  na mrs will smith mama wa watoto  wawili Jaden na Willow alitakiwa kufanya mapenzi na rapa 2pac yaani “really sex” lakin ilishindikana kwasababu 2pac alikataa kupima HIV


  6.LIL WAYNE KUJIPIGA RISASI MWENYEWE
    Dwayne Carter raper na CEO wa YMCMB a.k.a Lil Wayne alishawahi ji-shoot mara mbili lakini Weezy hajawa specific kama ni bahati mbaya au makusudi…
  
7.ISSUE YA DR DRE NA BANGI
   Dr dre ni producer na CEO wa beats hearphones pamoja na head phones amesema kwa mara ya kwanza alianza kuvuta bangi a.k.a msuba  alipo kutana na SNOOP LION.. kwaiyo inawezekana jamaa alifundishwa na  2013 BET HIP HOP AWARDS host Snoop mara tu walipo kutana na Dr. Dre wakati anatoa nyimbo ya “strait outta Compton” ambayo ndani yake ali-rap kwamba “I don’t Smoke WEED or CESS” alikuwa hadanganyi kwani paka muda huo alikuwa hajawahikutana na  Snoop Lion

8.NAS KUACHA SHULE
   Unaweza cheka sana ukiskia hii na huwezi amini kwa upande mwengine pia lakini ndo ukweli wenyewe kwamba rapper Nas es cobar aliacha shule akiwa “grade 7” kibongo bongo ni darasa la saba.

 9.LIST YA RAPPERS WALIO SOMA PAMOJA
     Kama hujawahi jua Jay z na  Busta Rhymes wamesoma shule moja na wali-battle kwa mara ya kwanza wakiwa shuleni  shule yao iliitwa Cafeteria.. na pia shule hiyo hiyo waliwahi soma DMX na BIGGIE

10.ALBAM YA JAY Z “BLUE PRINT”
     Kama una presha usisome hii habarí maana inashtua kidogo kama unaijua album ya Jay z inayoitwa “blue print” Ambayo MTV walii-list kama album ya 500 katika album za karne 2000 album hiyo iliandikwa kwa siku mbili tuu

Monday, April 14, 2014

MAALIMU MUHIDIN GURUMO AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 74.


Mwanamuziki mkogwe wa muziki wa dance Nchini Maalim Muhidin Gurumo afariki dunia jumapili ya April 13baada ya kulazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam..

Mzee Gurumo alipelekwa kulazwa jumumosi hii katika hospitali hiyo na kulazwa wodi namba tano baada ya mapafu yake kujaa maji,ambapo awali alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali kiasi cha kulazwa katika hospitali hiyo lakini aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu.

Mzee Gurumo alizaliwa mwaka 1940 katika kijiji cha Masaki Kisarawe mkoa wa Pwani
Mwanamuziki huyo aliyeimbia bendi ya  Msondo Ngoma kwa zaidi ya miaka 50 tangia mwaka 1964, ameacha mjane na watoto.... extreme taarifa inawapapole familia ya mzee Ngurumo.
 
Blogger Templates