Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

Christian Bella asema sababu akatunga 'Nani Kama Mama'

 
Mwimbaji wa dansi, Christian Bella ameeleza kuwa alimshuhudia mkewe akijifungua, kitu kilichomfanya aandike wimbo wa ‘Nani Kama Mama’ aliomshirikisha Ommy Dimpoz. Christian Bella ambaye ni kiongozi wa Malaika Band ameeleza hayo wakati akiongea na gazeti la Mwanaspoti.
“Mwaka 2012 nilienda Sweden kwa mke wangu ambaye alikuwa anajifungua hivyo nililazimika kuwepo ili kushuhudia mtoto wangu akizaliwa .Nilishuhudia kila kitu na sasa nina watoto wawili wa kiume Jordan (7) na Hance (2).” Amesema Christian Bella.
“Niliamua kutunga wimbo huu baada ya kushuhudia hatua zote mke wangu alipojifungua, kiukweli mwanamke anatakiwa kuheshimika tofauti na wanavyowachukulia, hapo ndipo niliona kuna haja ya kuimba wimbo wenye ujumbe huu.”

Shilole kuwania ubunge wa Igunga


Inawezekana kabisa Shilole akawa msanii ambaye ungedhani angewekeza zaidi kwenye duka la urembo, nguo ama hata madini kwa jicho la kawaida kama akitaka kufanya biashara mbali na muziki. Lakini kwa jicho la tatu usimchukulie hivyo.

Msanii huyo ambaye ni mzaliwa wa Igunga  panapofahamika zaidi kama kwa Rostam Aziz, mbunge aliyekaa muda mrefu madarakani kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Kafumu ambaye ni mbunge wa sasa, amepanga kuingia kwenye mchakato wa ubunge kwa lengo la kulitwaa jimbo hilo.
Shilole aliiambia Bongo Dot Home kuwa amefanya uamuzi wa kugombea katika jimbo hilo kwa kuwa anaona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa na yeye kama mzawa anaamini anaweza kuwasaidia zaidi wananchi wa Igunga.
“Ni kwa sababu ya matatizo yaliyopo. Nimekuwa nikienda naona matatizo kila siku yapo..ndio maana naona kama naweza kusimama na watu wengi sana wakanisikiliza kwa nini nisijitokeze kuwasaidia matatizo yao. Nimezaliwa pale mimi, nakijua kitongoji kimoja baadaya kingine.” Ameeleza.
“Nikipata ubunge kwanza kabisa nitadeal na akina mama, wafanyabiashara ndogondogo waweze kujikwamua vizuri. Pili vijana waweze kupata ajira kwa sababu sasa hivi naona vijana wa Igunga ajira zimekuwa ngumu kupatikana. Kuweka vitendea kazi ambavyo vitakuwa rahisi sana kuweza kufanya kazi na kutoa vijijini kupeleka mjini.” Alijinadi Shilole.
Akiwa kwenye kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm, mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na muziki yeye ni mkulima wa mpunga na ana mashamba mengi ya mpunga huko Igunga.

Monday, August 4, 2014

Collabo ya Davido na Drake hii hapa..


Msanii wa Nigeria, Davido anaendelea kusaka nafasi ya kuwa kati ya wasanii wakubwa zaidi sio tu Afrika bali dunia nzima kwa ujumla.
Siku kadhaa baada ya kutangaza collabo na Meek Mill na Rick Ross, mwimbaji huyo wa ‘Aye’ ameiambia Encomium kuwa yuko katika mazungumzo na rapper wa Young Money, Drake kwa ajili ya kufanya collabo kwa usimamizi wa Don Jazzy.
“I might not call it ‘dream collaboration’ but by His grace, it’ll work, and already, I am talking with Drake and Don Jazzy. We would work on something very unique.” Amesema Davido.
Amefafanua kuwa mpango wake wa kufanya collabo na wasanii wakubwa wa kimataifa au hata wadogo sio kwa lengo la kusaka umaarufu.
“My collaboration with other artistes is not a ploy to be popular, after all, I am not going to take the glory alone. Apart from the artistes you collaborated with, you never know what song can make you big as well. It doesn’t matter if you feature a big or up-and-coming artiste. That’s the main reason I am doing this.”

Maneno ya Ay baada ya kufika Ikulu Marekani na alichokutana nacho

A.Y tayari ameshafika Marekani na wameanza kwa kukutana na Wafanyakazi wa ofisi ya Rais Barack Obama ambapo msafara huo wa wasanii wa Afrika umepata nafasi ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani ya White House ikiwemo ofisi ya Obama inayoitwa Oval.


Huu msafara wa wasanii kutoka Africa unajumuisha Femi Kuti, D Banj wa Nigeria, Victoria Kimani wa Kenya, Buffalo Soldier wa Zimbabwe na A.Y ambapo kesho wanatarajia kukutana na Rais Barack Obama.


Baada tu ya kufika, Ay kaniambia kitu cha tofauti alichokutana nacho kwenye Ikulu hii ni kwamba jamaa wanakwenda na dress code kutokana na siku, yani imepangwa kuna mavazi ya kuvaa kutokana na siku… kwa weekend ambayo Ay na wenzake waliitembelea Ikulu mtu yeyote haruhusiwi kuvaa suti hivyo utawakuta Wafanyakazi wengine na kaptula au jeans.
Hata kina Ay wakati wanajiandaa kwenda Ikulu waliambiwa wasivae suti maana ni weekend.

Ay anasema kingine ni kwamba Obama kila wiki anatenga siku ya kukutana na Watoto kutoka sehemu mbalimbali wanaotembelea Ikulu.

Thursday, July 24, 2014

Brand New Song: Country Boy Ft. Blue Mchaka Mchaka


Hii ni ngoma nyingine mpya kutoka kwa Country Boy inaitwa Mchaka Mchaka, ngoma imefanyika chini ya producer Messen Selekta,
Blue ameisimamia vya kutosha chorus ya ngoma hii…
Bonyeza hapa kusikiliza

Tuesday, May 6, 2014

FID Q "NILISTAHILI KUSHINDA TUZO YA KILL, KILA MTU AMEFURAHI BAADA YA KUNIBANIA KWA MUDA MREFU"



Msanii Fid Q amehabarisha kuwa kila mtu amefurahi kwa yeye kushinda Tuzo ya Mwana Hip Hop Bora wa Mwaka , Amesema hiyo inajidhihirisha hata kwenye Social Media kila mtu anasifia na kukubali ishindi wake
                          ..Amasema Amebaniwa Miaka Mingi hiyo tuzo na Hatimae ameipata....

Saturday, May 3, 2014

Hatimaye KTMA 2014 hii hapa, leo usiku


Wahenga wanasema subira yavuta heri. Hilo linathibitishwa, baada ya kusubiri kwa miezi zaidi ya mwili hatimaye leo ndio tuzo kilele cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.


Fuatilia kila tukio live kupitia www.kililager.com/KTMA ukianza na Red Carpet wakati Jokate Mwegelo, Salma Msangi na Millard Ayo wakiwahoji mastaa mbalimbali watakaokuwa wakiwasili katika zuria jekundu na utaweza kujua kina nani wametokezea. Baadae wataungana na Sam Misago wa EATV katika Social Media Lounge ambapo wakuwa wakiwahoji washindi na wateule wengine wa tuzo.

Thursday, May 1, 2014

VIDEO: Sauti sol - Nishike hii hapa

Baada ya skendo nyingi kwa wanamuziki wa kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya, sasa watoka na song jipya kwa jina la "Nishike" kuonesha kuwa

Wednesday, April 30, 2014

Wema Sepetu na Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza rasmi kuwa kwa jukwaa moja

Inawezekana uliwahi waona kwenye matamasha mbalimbali Wema Sepetu na Diamond wakiwa pamoja lakini hua inakua kama ‘Sapraiz’ ili pengine kuleta hamasa kwa mashabiki wao,sasa rasmi hii ni show ya kwanza ambayo itamueka Diamond Platnumz na Wema Sepetu kwenye jukwaa moja.
Wakazi wa Mtwara wamepata zali hili la kuona mastar hawa wakiwa wanaupeleka usiku wa Hills and Tie ambao umedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom,Meneja Masoko wa Vodacon Kelvin Twissa amesema huu utakua mkoa wa Kwanza na kama Mtwara watatoa sapoti wanategemea kuifanya iwe tour. Hii ni namba maalum kwa ajili ya wateja wa vodacom kuweza kununua tiketi kupitia M pesa kwa simu zao za mkononi ambapo kwa yeyote atakaenunua atapata punguzo la asilimia 20 namba hiyo ni 0754 980 769.



Monday, April 28, 2014

WIMBO ULIOWAKUTANISHA WASANII 50 KUTOKA TANZANIA

Wimbo Maalumu wa Muungano ulioimbwa na wasanii 50 kutoka Tanzania ambao kwa pamoja walikaa na kutengeneza wimbo huu,jina la wimbo huu unaitwa Tuulinde umetayarishwa na maproducer wawili Ema the boy na Tuddy Thomas kutoka Soround Sound Studio.


Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki wa hapa Tanzania kuna wa Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili.
Inawezekana ikawa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja,kwa ushirikiano mkubwa,wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu.
Miongoni mwa wasanii ambao utazisikia sauti zao ni pamoja na Kadjanito,Mwasiti,Linah,Christina Shusho,Khadija Kopa,Frola Mbasha,Ommy Dimpoz,Diamond,Josse Mara,Kalala Jr,Ali Kiba,Peter Msechu,Mrisho Mpoto,Abdul Kiba,Mzee Yusuph,Angel,Mwana Fa,Nikki Wa pili,G Nako,God Zilla,Madee,Asley,Shaa,Mandojo,Domokaya,Shilole na Roma Mkatoliki.

USIKU WA MKETE FASHION MBEYA

Usiku uliojaa ubunifu na burudani mbalimbali ndani ya ukumbi wa Mtenda Sunset, na kuacha uzoefu  wa kitofauti kwa wakazi wa Mbeya kwani haijawahi tokea fashion show kama hiyo mkoani humo....kama ilivyo pangwa usiku huo ulipambwa na Designer na Models kutoka vyuo vikuu vya Mbeya na pia kutoka Green team photogenic.
Mgeni rasmi,sponsors na waandaaji wa mkete fashion night
Designers na Models wakijiaanda



Na pia wasanii na ma dancers walokuwepo na kuleta radha nyingine poa sana ndani ya usiku wa Mkete fashion.... mashabiki waliburudishwa zaidi na sauti nzuri ya msanii kutoka Mbeya Modolist kwenye usiku huu
Washiriki na wazamini wa fashion show hiyo pia walipewa vyeti vya ushiriki katika usiku wa Mkete





Mkete fashion night ndani ya Mbeya hufanyika kila mwaka kuanzia mwaka 2014 na kuendelea...
kwa matukio mengine ya like page yetu Extreme Taarifa

Thursday, April 24, 2014

Ni ghafla lakini hii hapa MKETE FASHION NIGHT 2014 Mbeya


Usiku wa Fashion ndani ya ukumbi wa Mtenda hall siku ya jumamosi 26, April,2014 sasa umefika kwa mtu yeyote anakaribishwa katika usiku huu uliojaa fun na  ubunifu kutoka kwa Designers na Models wa Mbeya.. hii sio ya kukosa jamaa
Burudani mbalimbali zaidi ya fashion show zitaletwa kwenyu na vijana wa mbeya na pia wanachuo kutoka Mzumbe,MUST,TIA,CDTI na TEKU ili kuusindikiza usiku huo wa ubunifu..

Tuesday, April 22, 2014

KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P-SQUARE


Wiki hii mitandao ya Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa kati ya mapacha wanaounda kundi la PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.

Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.

Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo.

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.” Alitweet Jude Okoye.

Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha habari hizo wakati akiongea na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi. 

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.” Amesema Bayo Adetu.

Thursday, April 17, 2014

TEN HIP HOP FACTS HIZI HAPA

HIP HOP ni aina ya muziki au utamaduni unaopendwa na vijana wengi zaidi duniani na ni aina ya muziki wenye mashabiki wengi zaidi… kuna baadhi ya mambo ambayo najua utakua haufahamu kuhusiana na muziki huu na hujawahi sikia kwa mtu sasa fungua macho nikupe ukweli wa mambo kadhaa..

1.KUNDI LA HIP HOP LA KWANZA LA WANAWAKE
      Tumeona makundi mengi ya hip-hop huwa ni ya wanaume tupu lakini hawa ndio wanawake wa kwanza kuwa pamoja na kutengeneza group moja lililokwenda kwa jina la MARCEDES LADIES

2.KAZI ALIYOFANYA DIDDY KABLA YA KUANZA MUZIKI
     Kwa mara ya kwanza P.diddy alianza kuonekana katika majukwaa ya HIP HOP  akiwa kama “back up” dancer wa Big Daddy Kane.. hapo ndio tunaona kweli everything Start from bottom

3.MARA YA KWANZA JAY Z KU-SHOOT MTU
     Moja kati ya wana hip hop wajasiriamali wenye vitega uchumi vingi nchini Marekani na dunia nzima.. Jigga alianza kupenda pesa akiwa mdogo na hii inaonyesha kuwa Jigga anapenda pesa kuliko utu.. Jigga kachafua biography yake baada ya kum-shoot his blood brother yaani tumbo moja baada ya kumuibia mtonyo tu.

4. PROJECT YA PEKEE ILIYO MPATIA NAS TUNZO YA GRAMMY
     Project ya kwanza naya mwisho ya Nas kunyakua au kubeba tunzo ya grammy… ni ile aliyo muandikia Will Smith nyimbo inaitwa “jiggy with it” Nas hajawahi pata tunzo ya grammy tena tangu project hiyo… Damn Nas!! If I was ur pop ALU DARA I could ask you to stop raping *KIDING*

5.POETIC JUSTICE SEX SCENE
   Kama hujawahiona filamu ya “poetic justice” nakusihi ukaitafute bonge la filamu hilo kuwa na mastaa kibao ndani yake movie hii ilikua ikizungumzia maisha ya mtu mweusi hasa vijana waishio Marekani ndani yake kulikua na Janet Jackson na pia one of the best rapper of all time 2PAC SHAKUR
      Sasa  wakati wa uandaaji wa movie hiyo kuna scene ambayo  2pac na Janet Jackson  na mrs will smith mama wa watoto  wawili Jaden na Willow alitakiwa kufanya mapenzi na rapa 2pac yaani “really sex” lakin ilishindikana kwasababu 2pac alikataa kupima HIV


  6.LIL WAYNE KUJIPIGA RISASI MWENYEWE
    Dwayne Carter raper na CEO wa YMCMB a.k.a Lil Wayne alishawahi ji-shoot mara mbili lakini Weezy hajawa specific kama ni bahati mbaya au makusudi…
  
7.ISSUE YA DR DRE NA BANGI
   Dr dre ni producer na CEO wa beats hearphones pamoja na head phones amesema kwa mara ya kwanza alianza kuvuta bangi a.k.a msuba  alipo kutana na SNOOP LION.. kwaiyo inawezekana jamaa alifundishwa na  2013 BET HIP HOP AWARDS host Snoop mara tu walipo kutana na Dr. Dre wakati anatoa nyimbo ya “strait outta Compton” ambayo ndani yake ali-rap kwamba “I don’t Smoke WEED or CESS” alikuwa hadanganyi kwani paka muda huo alikuwa hajawahikutana na  Snoop Lion

8.NAS KUACHA SHULE
   Unaweza cheka sana ukiskia hii na huwezi amini kwa upande mwengine pia lakini ndo ukweli wenyewe kwamba rapper Nas es cobar aliacha shule akiwa “grade 7” kibongo bongo ni darasa la saba.

 9.LIST YA RAPPERS WALIO SOMA PAMOJA
     Kama hujawahi jua Jay z na  Busta Rhymes wamesoma shule moja na wali-battle kwa mara ya kwanza wakiwa shuleni  shule yao iliitwa Cafeteria.. na pia shule hiyo hiyo waliwahi soma DMX na BIGGIE

10.ALBAM YA JAY Z “BLUE PRINT”
     Kama una presha usisome hii habarí maana inashtua kidogo kama unaijua album ya Jay z inayoitwa “blue print” Ambayo MTV walii-list kama album ya 500 katika album za karne 2000 album hiyo iliandikwa kwa siku mbili tuu

Monday, April 14, 2014

MAALIMU MUHIDIN GURUMO AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 74.


Mwanamuziki mkogwe wa muziki wa dance Nchini Maalim Muhidin Gurumo afariki dunia jumapili ya April 13baada ya kulazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam..

Mzee Gurumo alipelekwa kulazwa jumumosi hii katika hospitali hiyo na kulazwa wodi namba tano baada ya mapafu yake kujaa maji,ambapo awali alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali kiasi cha kulazwa katika hospitali hiyo lakini aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu.

Mzee Gurumo alizaliwa mwaka 1940 katika kijiji cha Masaki Kisarawe mkoa wa Pwani
Mwanamuziki huyo aliyeimbia bendi ya  Msondo Ngoma kwa zaidi ya miaka 50 tangia mwaka 1964, ameacha mjane na watoto.... extreme taarifa inawapapole familia ya mzee Ngurumo.

BREAKING NEWS:bomu lililolipuka Arusha April 13 usiku, idadi ya waliojeruhiwa.


Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.

Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.

Sunday, April 13, 2014

255 EXCLUSIVE: MODOLIST - USINIACHE

Bonge la song kutoka kwa msanii from Greencity, Mbeya city... ni wimbo unaofanya vizuri sana kutokana na mahudhui na uimbaji wa underground huyo anayefahamika kwa jina la Modolist, akiyalilia mapenzi au mpenzi
sikiliza na kudownload hapa....

Artist;Modolisti
Song ;Usiniache
SIKILIZA NA DOWNLOAD HAPA

Saturday, April 12, 2014

VIDEO:ONE - COCOA NA CHOCOLATE HII HAPA

Song iliyowakusanya wanamuziki wakubwa kutoka Africa akiwemo na Rais wa wasafi Diamond platnumz na pia Ambwene Yesaya kutoka Tanzania ndani ya kichupa hiki...

BEHIND THE SCENE VIDEO:QUEEN DARLEEN FET. SHILOLE - WANATETEMEKA HII HAPA

Hii ni video iliyowahusisha Diamond Platnumz na dada yake wa damu  Queen Darlin uzinduzi wa video hii ulifanyika Bilicanas mwishoni mwa wiki iliyopita,video hii imetenegezwa na kampuni ya Jerry Mushala Studio.

VIDEO: YEMI ALADE - JOHNNY HII HAPA

Tazama hii hapa video mpya ya mwanadada Yemi Alade kutoka Nchini Nigeria, akifanya vizuri zaidi katika nyimbo hiyo iliyotamba sana East Africa na Afrika kiujumla..
 

Thursday, April 10, 2014

Lupita Nyong'o akava jarida la Marie Claire

Ikiwa ni wiki moja tuu toka mwanadada nyota wa filamu ya "12 years of slave" Lupita Nyong'o kutangazwa kuwa ni balozi wa vipodozi vya Lincome ya Ufaransa, mwigizaji huyo amekava jarida la Marie Claire toleo la mwezi ujao ( may 2014)..

Katika jarida hilo mwigizaji huyo wa kenya amezungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na projects zake zijazo.Pia amekiri kuwa hapo mwanzo hakuwa mtu wa fashion na kumpa sifa na shukrani stylist wake Micaela Erlanger ambaye ndiye husimamia swala zima la muonekano wake.

MAJINA YA WANAMUZIKI WANAOWANIA "NOMINEES" TUZO ZA BILLBOARD MUSIC AWARDS HAYA HAPA



Majina ya wanamuziki hao yametangazwa rasmi April 9, na mastar wenye kuwania category nyingi zaidi katika tunzo hizo ni Imagine Dragons na Fellow Finalist Lorge wakiongoza kwa nomination katika categories 12, wakifuatiwa na mwanamuziki Justin Timberlake akiwa na nomination 11 na pia mwanadada Katy pery akiwa na nomination 10.... na hapa ni wasanii na bandi katika categories zinazowania tunzo za Billboard Music Awards


MWANAMUZIKI BORA
Miley Cyrus
Imagine Dragons
Bruno Mars
Katy Perry
Justin Timberlake



MSANII BORA WA KIUME
Luke Bryan
Drake
Eminem
Bruno Mars
Justin Timberlake

MSANII BORA WA KIKE
Beyonce
Miley Cyrus
Lorde
Katy Perry
Rihanna

KUNDI BORA
Florida Georgia Line
Imagine Dragons
Macklemore & Ryan Lewis
One Direction
OneRepublic

Top Billboard 200 Artist
Beyonce
Luke Bryan
Eminem
One Direction
Justin Timberlake

Top Hot 100 Artist
Miley Cyrus
Imagine Dragons
Lorde
Katy Perry
Justin Timberlake

Top Digital Songs Artist
Miley Cyrus
Imagine Dragons
Lorde
Macklemore & Ryan Lewis
Katy Perry

Top Radio Songs Artist
Imagine Dragons
Lorde
Bruno Mars
Katy Perry
Justin Timberlake

Top Touring Artist
Beyonce
Bon Jovi
Pink
Rihanna
Bruce Springsteen & the E Street Band

Top Social Artist
Justin Bieber
Miley Cyrus
One Direction
Rihanna
Taylor Swift

Top Streaming Artist
Miley Cyrus
Imagine Dragons
Macklemore & Ryan Lewis
Katy Perry
PSY

Top R&B Artist
Beyonce
Pharrell
Rihanna
Robin Thicke
Justin Timberlake

Top Rap Artist
Drake
Eminem
Jay Z
Macklemore & Ryan Lewis
Pitbull

Top Country Artist
Luke Bryan
Florida Georgia Line
Darius Rucker
Blake Shelton
Taylor Swift

Top Rock Artist
Capital Cities
Fall Out Boy
Imagine Dragons
Lorde
Passenger

Top Latin Artist
Marc Anthony
Gerardo Ortiz
Jenni Rivera
Prince Royce
Romeo Santos

Top Dance / Electronic Artist
Avicii
Daft Punk
Calvin Harris
Lady Gaga
Zedd

Top Christian Artist
Mandisa
Skillet
tobyMac
Chris Tomlin
Matthew West

ALBUM AWARDS

Top Billboard 200 Album
Beyonce - "Beyonce"
Luke Bryan - "Crash My Party"
Drake - "Nothing Was The Same"
Eminem - "The Marshall Mathers LP 2"
Justin Timberlake - "The 20/20 Experience"

Top R&B Album
Beyonce - "Beyonce"
R. Kelly - "Black Panties"
Robin Thicke - "Blurred Lines"
Justin Timberlake - "The 20/20 Experience"
Justin Timberlake - "The 20/20 Experience (2 of 2)"

Top Rap Album
J. Cole - "Born Sinner"
Drake - "Nothing Was The Same"
Eminem - "The Marshall Mathers LP 2"
Jay Z - "Magna Carta& Holy Grail"
Macklemore & Ryan Lewis - "The Heist"

Top Country Album
Garth Brooks - "Blame It All On My Roots: Five Decades of Influences"
Luke Bryan - "Crash My Party"
Florida Georgia Line - "Here's To The Good Times"
The Robertsons - "Duck The Halls: A Robertson Family Christmas"
Blake Shelton - "Based On A True Story"

Top Rock Album
Lana Del Rey - "Born To Die"
Fall Out Boy - "Save Rock And Roll"
Imagine Dragons - "Night Visions"
Lorde - "Pure Heroine"
Mumford & Sons - "Babel"

Top Latin Album
Marc Anthony - "3.0"
Alejandro Fernandez - "Confidencias"
Jenni Rivera - "1969 - Siempre: En Vivo Desde Monterrey: Parte "
Prince Royce - "Soy El Mismo"
Romeo Santos - "Formula: Vol. 2"

Top Dance / Electronic Album
Avicii - "True"
Daft Punk - "Random Access Memories"
Lady Gaga - "ARTPOP"
Lindsey Stirling - "Lindsey Stirling"
Zedd - "Clarity"

Top Christian Album
Alan Jackson - "Precious Memories: Volume II"
Skillet - "Rise"
Third Day - "Miracle"
Chris Tomlin - "Burning Lights
Various Artists - "WOW Hits 2014"

SONG AWARDS

Top Hot 100 Song
Miley Cyrus - "Wrecking Ball"
Imagine Dragons" - "Radioactive"
Lorde - "Royals"
Katy Perry - "Roar"
Robin Thicke Featuring T.I. & Pharrell - "Blurred Lines"

Top Digital Song
Imagine Dragons - "Radioactive"
Lorde - "Royals"
OneRepublic - "Counting Stars"
Katy Perry - "Roar"
Robin Thicke Featuring T.I. & Pharrell - "Blurred Lines"

Top Radio Song
Avicii - "Wake Me Up"
Lorde - "Royals"
Katy Perry - "Roar"
Robin Thicke Featuring T.I. & Pharrell - "Blurred Lines"
Justin Timberlake - "Mirrors"

Top Streaming Song (Audio)
Daft Punk Featuring Pharrell William - "Get Lucky"
Imagine Dragons - "Radioactive"
Lorde - "Royals"
Macklemore & Ryan Lewis Featuring Ray Dalton, "Can't Hold Us"
Robin Thicke Featuring T.I. & Pharrell - "Blurred Lines"

Top Streaming Song (Video)
Baauer - "Harlem Shake"
Miley Cyrus - "We Can't Stop"
Miley Cyrus - "Wrecking Ball"
Macklemore & Ryan Lewis Featuring Wanz - "Thrift Shop"
Katy Perry - "Roar"

Top Rap Song
Eminem Featuring Rihanna - "The Monster"
Jay Z Featuring Justin Timberlake - "Holy Grail"
Macklemore & Ryan Lewis Featuring Ray Dalton - "Can't Hold Us"
Macklemore & Ryan Lewis Featuring Wanz - "Thrift Shop"
Pitbull Featuring Ke$ha - "Timber"

Top Country Song
Luke Bryan - "Crash My Party"
Luke Bryan - "That's My Kind Of Night"
Florida Georgia Line Featuring Nelly - "Cruise"
Darius Rucker - "Wagon Wheel"
Blake Shelton Featuring Pistol Annies & Friends - "Boys 'Round Here"

Top Rock Song
Capital Cities - "Safe And Sound"
Imagine Dragons - "Demons"
Imagine Dragons - "Radioactive"
Lorde - "Royals"
Passenger - "Let Her Go"

Top Latin Song
Marc Anthony - "Vivir Mi Vida"
Daddy Yankee - "Limbo"
Enrique Iglesias Featuring Romeo Santos - "Loco"
Prince Royce - "Darte Un Beso"
Romeo Santos - "Propuesta Indecente"

Top Dance / Electronic Song
Avicii -"Wake Me Up"
Daft Punk Featuring Pharrell Williams - "Get Lucky"
Icona Pop Featuring Charlie XCX - "I Love It"
Lady Gaga - "Applause"
Zedd Featuring Foxes - "Clarity"

Top Christian Song
Building 429 - "We Won't Be Shaken"
Mandisa - "Overcomer"
Sidewalk Prophets - "Help Me Find It"
Chris Tomlin - "Whom Shall I Fear (God Of Angel Armies)"
Matthew West - "Hello, My Name Is"

Monday, April 7, 2014

MASTAR WENYE MASHABIKI WENGI MTANDAONI.

Leo tunakuletea list ya ma star watano wanaoongoza katika social network, listi hii inakusanywa na mtandao wa swahilitz kuanzia kwenye facebook, twitter na instagram ni msanii gani anaongoza kati ya wote hapa bongo. Vigezo vilivyotumika kuwapata top 5 hii ni idadi ya juma ya mashabiki wa wasanii hawa katika mitandao yote mitatu na kisha kupata wastani wa mashabiki
 Well wacha tuanze list hii tukianza na namba moja hadi 5, unadhani ni nani kaongoza katika list hii fatilia hapa..



 1. Lady Jay Dee aka Komando aka Anaconda.
Judith Wambula likiwa ndiyo jina lake halisi la kwenye kitambulisho ila jina la kisanii anajulikana kama Lady Jay Dee, ni msanii wa kike aliyetamba katika game karibia miaka 15 mpaka sasa tangu aanze muziki na ndiye star anayeongoza kuwa na mashabiki wengi zaidi katika social network. katika ukurasa wake wa facebook Lady Jay Dee ana like zaidi ya 262,583 huku katika akaundi yake ya twitter ana followers zaidi ya 76k na instagram ana follower 27,520 huku akiwa na wastani wa mashabiki 122034.3 katika mitandao yote mitatu ya kijamii

                                             




                      






 2, Diamond Platnumz aka Dangote
                                                  
Jina la kwenye ID ni Naseeb Abdul ila linalompa kula ni Diamond Platunumz, kwa upande wa muziki wa bongo fleva huyu ndiye msanii anayelipwa Pesa nyingi zaidi kwa kila show anayofanya iwe ndani au nje ya Bongo na kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kujiongezea umaarufu na umaarufu unapanda zaidi kutokana na mahusiano ya kimapenzi aliyonayo na mtoto wa marehemu mzee Sepetu, Diamond anashika nafasi ya pili akiwa na likes 164,665 katika facebook na twitter ana followers zaidi ya 62.9k, huku instagram akiwa na followers zaidi ya 101k huku instagram akiwa na followers 43,678 huku akiwa na wasani wa mashabiki 109521.7 katika mitandao yote mitatu ya ya kijamii

                 



 





 3. Masanja Mkandamizaji aka Mchungaji
                              
     
Jina la kwenye kitambulisho ni Emanuel Mgaya ila anajulikana kama Masanja Mkandamizaji, umaarufu wake ulianza alipokuwa akifanya kipindi cha comedy katika kituo cha channel 5 na baadae kuhamia TBC1 katika kipindi chote hicho Masanja anahesabika kuwa ni miongoni mwa wachekeshaji wakubwa zaidi hapa Tanzania. Masanja anashika nafasi ya tatu katika countdown yetu huku akiwa na likes 200,177  katika ukurasa wake wa Facebook huku katika twitter akiwa na follower zaidi ya 91.1k na instagram ana follower 16,448 huku akiwa na wasani wa mashabiki 102575 katika mitandao yote
mitatu  ya kijamii

                                             











 4. Millard Ayo aka Mtu wangu wa Nguvu
                   
Siku baada ya siku jina lake linazidi kukuwa hasa akiwa ndiye kijana anayewavutia watu wengi wa kila lika kwa namna ya utangazaji wake na muonekano wake kwa ujumla. Millard Ayo ni mtangazaji wa Clouds anayekuwa na kipindi kila siku za wiki kuanzia saa 1 kamili hadi saa3 usiku akiwa anahesabu habari 10 za moto za ndani na nje ya bongo. Millard Ayo anashika nafasi ya 4 akiwa na jumla ya likes 169,298 katika facebook na twitter ana followers zaidi ya 87.7k, huku instagram akiwa na followers 43,678 huku akiwa na wasani wa mashabiki 100225.3 katika mitandao yote mitatu ya kijamii

                                               








                         







  5.Wema Sepetu aka Madame

     
Jina la wema limekuwa gumzo kila kukicha katika social media na kwenye magazeti ya udaku kwani kila siku lazima awepo katika magazeti hayo. Wema sepetu ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mwanamziki Diamond Platnumz. Wema anajumla ya likes 82,651 kwenye facebook na twitter ana followers zaidi ya 65.9k huku instagram akiwa na followers 88,683 huku akiwa na wasani wa mashabiki 79,078 katika mitandao yote mitatu ya  kijamii



                            
                                                            

Tuesday, March 25, 2014

MAJINA YA WASANII WANAOWANIA "NOMINEES" TUNZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC 2014


Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza rasmi matokeo ya mchakato wa kuwapata wateule rasmi yaani ‘nominees’ wa vipengele 34 vya tuzo za muziki Tanzania.HAWA HAPA..

Wimbo Bora wa mwaka
Number One – Diamond
Joto Hasira – Jaydee
I love u – Cassim
Yahaya – Lady Jaydee
Kidela – Abdul Kiba
Muziki Gani – Nay wa Mitego

Wimbo bora wa Kiswahili – Band
Ushamba Mzigo – Mashujaa
Shamba la Bibi – Victoria sound
Chuki nini – FM Academia
Yarabi nafsi – Mapacha 3
Kiapo – Talent Band

Wimbo Afro Pop
Number One – Diamond
Joto Hasira – Lady Jaydee
Kidela – Abdul Kiba
I love u – Cassim
Tupogo – Ommy Dimpoz
Roho Yangu – Mavoko

Wimbo bora wa Hip Hop
Bei ya Mkaa – Weusi
Nje ya Box – Nick wa Pili & Joh Makini
Siri ya Mchezo – Fid Q
2030 – ROMA
Pesa – Mr Blue

Wimbo bora wa R&B
Listen – Belle 9
Closer – Vanessa Mdee
So Crazy – Maua Samma
Kama Huwezi – Rama Dee
Wa Ubani – Ben Pol

Wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana
Muziki Gani – Nay wa Mitego f/ Diamond
Joto Hasira – Lady Jaydee f/ Profesa Jay
Kidela – Abdul Kiba f/ Ali Kiba
Bila Kukunja Goti – Mwana FA & AY f/ J-Martins
Tupogo – Ommy Dimpoz f/ J-Martins

Wimbo bora wa Zouk Rhumba
Yahaya – Lady Jaydee
Yamoto – Mkubwa na Wanawe
Msaliti – Christian Bella
Nakuhitaji – Malaika Band
Narudi Kazini – Beka

Mwimbaji Bora wa Kike – Kizazi Kipya
Vanessa Mdee
Lady Jaydee
Linah
Maua Sama

Mwimbaji Bora wa Kiume Kizazi Kipya
Ben Pol
Rich Mavoko
Diamond Platnumz
Ommy Dimpoz
Cassim Mganga

Msanii Bora Hip Hop
Fid Q
Stamina
Young Killer
Nick wa Pili
G-Nako

Msanii Bora Chipukizi
Young Killer
Walter Chilambo
Y Tony
Snura
Meninah

Mtayarishaji Bora – Kizazi Kipya
Marco Chali
Man Water
Mazoo
Sheddy Clever
Nahreel

Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya
Belle 9
Ben Pol
Diamond
Rama Dee
Rich Mavoko

Mtunzi Bora Hip Hop
Nikki wa Pili
Young Killer
ROMA
Fid Q
G-Nako

Mtumbuizaji Bora wa Kiume Kizazi Kipya
Diamond
Christian Bella
Rich Mavoko
Ommy Dimpoz
Abdul Kiba

Video Bora ya Mwaka
Number One – Diamond
Yahaya – Lady Jaydee
Joto Hasira – Lady Jaydee
Uswazi Takeaway – Chege
Mama yeyo – GNako

Mtunzi Bora wa Mwaka Band
Christian Bella
Jose Mara
Chaz Baba
Nyosh El Saadat
Kalala Junior

Bendi ya Mwaka
FM Academia
Mapacha Watatu
Twanga Pepeta
Akudo Impact
Malaika Band
Mashujaa Band

Kikundi Cha Mwaka – Kizazi Kipya
Makomandoo
Navy Kenzo
Weusi
Mkubwa na Wanawe
Kikundi cha Mwaka – Taarab
Jahazi Modern Taarab
Mashauzi Classic
Five Stars

Mwimbaji Bora wa Kike – Taaarab
Khadija Kopa
Isha Ramadhani
Khadija Yusuph
Mwanahawa Ali
Leyla Rashid

Mwimbaji Bora Kiume – Taarab
Mzee Yusuf
Hashimu Saidi
Mohamed Ali aka Mtoto Pori

Mwimbaji Bora Kiume – Bendi
Jose Mara
Kalala Junior
Charz Baba
Khalid Chokoraa
Christian Bella

Mtunzi Bora Taarab
Mzee Yusuf
El-Ahad Omary
El-Khatib Rajab
Kapten Temba
Sadiki Abdul
Nassoro Seif

Rapper bora wa mwaka – Bendi
Kitokololo
Chokoraa
Ferguson
Canal Top
Totoo Ze Bingwa

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab
Enrico
Abuu Mwana ZNZ
Bakunde

Mwimbaji Bora wa Kike – Bendi
Luiza Mbutu
Catherine Cindy
Ciana

Wimbo bora wa reggae
Niwe Nawe – Dabo
Hakuna Matata – Lonka
Tell Me – DJ Aron f/ Fidempha
Bado Nahitaji – Chikaka f/ Bless P & Lazzy
Bongo Reggae -Warriors from the East

Wimbo bora wa Ragga/Dancehall
Nishai – Chibwa f/ Nuru
Sexy Girl – Dr Jahson
My Sweet – Jetman
Feel Alright – Lucky Stone
Wine – Princess Delyla

Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Tubonge – Jose Chameleone
Nakupenda Pia – Wyre f/ Alaine
Badilisha – Jose Chameleone
Kipepeo – Jaguar
Kiboko Changu f/ Radio and Weasel

VIDEO MPYA YA SHILOLE "CHUNA BUZI"

Video iliyoleta gumzo sana mtandaoni kutokana na matukio yaliyomo kwenye video hii...
   Shilole "Chuna buzi" video

Sunday, March 23, 2014

VIDEO MPYA LADY GAGA "G.U.Y" KUTOLEWA SASA

           Mwanamuziki mwenye vituko sana katika video zake Lady Gaga ameachia  video ya wimbo wake "G.U.Y ( Girl Under You )"video imeongazwa na yeye mwenyewe na ilifanyika kwa siku 6 huko California kwenye hekalu la Hearst Castle.
                                                              

SHAKIRA NDIYE MWANAMUZIKI MWENYE LIKES NYINGI ZAIDI KWENYE FACEBOOK,ZAIDI YA LIKES MILIONI 86

            Mwimbaji mrembo Shakira wa Colombia ndiye mwanamuziki mwenye ukurasa wenye likes au wafuasiwengi zaidi duniani kwa sasa katika mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kufikisha likes 86,549,479. Na kufuatiwa kwa karibu na mwanadada Rihanna aliyeshirikiana naye katika nyimbo iliyofanya vizuri sana "I can't remember to forget you" ambaye ameshika nafasi ya pili kwa kuwa na likes 86,200,046  hukuwa tatu ni mwanamuziki wa mziki wa HIP HOP Eminem mwenye likes 83,904,675 kwa mujibu wa metro.co.uk

Shakira
 Mwanadada Shakira mwenye hit song "Hips don't lie" pia alishare habari hiyo na mashabiki wake wa mtandao huo wa kijamii Facebook kwa kuandika;
"Wow.... i was just told i now have the most followed page on facebook in the world! i still cannot belive it!
i always wanted to have a lot of friends but never imagined it would be so many...86m!
so humbled,can't thanks you guys enough for your support,i feel so fortunate to have you.
Giant kiss! Forever thankful,
Shak
"

Shakira anatarajia kuachia album yake mpya na ya kumi iitwayo 'shakira' jumanne ya wiki hii inayoanza March 35.

Hii ni top ten ya watu maarufu wenye likes nyingi Facebook;
1.Shakira - 86,429,950 likes
2.Rihanna - 86,271,149 likes
3.Eminem - 83,935,160 likes
4.Cristiano Ronaldo - 76,148,074 likes
5.Michael Jackson - 71,605,480 likes
6.Vin Diesel - 70,124,905 likes
7.Katy perry - 65,694,061 likes
8.Will Smith - 64,732,390 likes
9.Justin Bieber - 64,167,390 likes
10.Lady Gaga - 63,776,645 likes

MBEYA FREE MUSIC CONCERT YA ZANTEL WAKISHILIKIANA NA SWEETY FM.

    Onesho lililofanyika mjini Mbeya katika viwanja vya "Mbeya city pub" na kupambwa na MCs kutoka sweety fm kwa ajili ya kukuza vipaji vya wasanii wanaochipukia mjini Mbeya .Msanii mkubwa wa mziki wa HIP HOP kutoka salasala Godzilla a.k.a King zilla ku-perform ndani ya jukwa hilo la Mbeya free music concert lililopambwa na vituko vingi kutoka kwa watoto wa Mbeya city....

Watangazaji wa Sweety fm Langa na Ashrey wakifungua show
 Show ilianzishwa na ma-underground, ma-dancers na wanamuziki kutoka Mbeya city waliovamia jukwaa kwa nguvu zote na kuacha mashabiki kupiga shangwe "non-stop" bila kuchokwa noa, kati ya wanaburudani walio pagawisha mashabiki ni Kareem,Z-kali,ukwu dancer na pia Modolist aliye pagawisha mashabikki zaidi  kwa wimbo wake wa "Usiniache" akifuatiwa na wanadada wa inye ndembendembe kupagawisha, pia burudani kutoka kwa watangazaji wa sweety fm kuwabamba zaidi mashabiki...

Watangazaji wa vipindi vya Sweety fm mbeya wakila bonge la sebene

Ukwu dancers nao hawakuwa nyuma katika kuwaburudisha mashabiki

Wadau wa burudani wakiwa wamefurahia show noma sana
Jukwaa lilipamba moto zaidi pale walipopanda wanamuziki kutoka Mbeya city wakifuatiwa na King zilla kutoka salasala Dar es salaam...wasanii waliokuwepo kutoka Mbeya city ni Kesse boy,Zax B,Jozy  mapenzi,PC the master,MC murder,Must,BZQ na pia mwanadada Lil stiga kwa pamoja ndani ya jukwaa moja na kuwapagawisha mashabiki sana.  

Friday, March 21, 2014

WIMBO MPYA WA LADY JAYDEE KUJA HIVI KARIBUNI

 Mwanamuziki Judith Wambura a.k.a Lady jaydee ameanza kuutangaza wimbo wake mpya unaoitwa  "nasimama" na kusema sio muda mrefu anaachia nyimbo hiyo baada ya "historia". Mwanadada huyo ambaye kabla ametesa sana na wimbo wa "yahaya" ameendelea kuwakimbiza wanamuziki wenzake kwa nyimbo "kistoria" na sasa "nasimama"

Lady Jaydee
Mwanadada huyo aanzakuitangaza wimbo huo kwa ku-post kwenye mitandao ya kijamii
"Chorus ya wimbo wangu mpya ambao haujatoka unaitwa NASIMAMA... maneno haya hapaa"

CHORUS;aliyepanga ni maanani,shida na riziki zangu
aliyezitupa gizani,shida na tabu zangu oooh *2

NYIMBO MPYA DIAMOND PLATNUMZ "KIFO CHANGU"

Mwanamziki namba 1 kwa kupiga show hapa Tanzania Diamond Platnumz hivi karibuni alitoa maneno akizungumza siku akifa itakuwawaje kitu ambacho kilizua maswali mengi sana kwa mashabiki wake ambao hawakutegemea hata siku moja kama atakuja kusema maneno kama hayo kwa mashabiki wake kwani yalizua mining'ono mingi sana. Katika kusema hayo maneno Diamond alisema ni moja kati ya nyimbo ambayo ameiandika na inamtoa machozi kia aisikapo.
Baadhi ya mashairi katika nyimbo hiyo alisema:

                                                 Vipi Maneke atanililia...??
                                                 Je wasanii wenzangu wataniimbia..??
                                                Ama litafutika jina langu...??
                                                Na nyimbo zangu hawatasikia..??
                                                Vipi wasafi watanililia....??
                                                Je ndugu rafiki watahudhuria..?? 
                                                Ama nitakapokufa Sina changu..??
                                               Hata mama yangu watamkimbia...??

Kwa mara ya kwanza pata kuisikiliza na kudownload nyimbo hiyo hapa Diamond-kifo-new song

Wednesday, March 19, 2014

YARIPOTIWA KUWA NCHINI MAREKANI VIJANA WENYE ASILI YA AFRIKA HUCHUKULIWA WANAHATIA.

   Makala iliyo sambazwa na "journal of personality and social psychology" imegundulika kuwa vijana wenye asili ya Africa nchini Marekani huchukuliwa kuwa ndio wenye vurugu na usumbufu katika sheria na kuwafanya kuwa wahanga wa matukio mbalimbali na bila kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya polisi kwasababu ya zana hiyo....



Polisi wa nchini Marekani wakimkamata kijana mwenye asili ya Afrika
        "Vijana katika jamii nyingi zinawachukulia vijana kama kundi la watu wasio na hatia na wanaitaji ulinzi kutoka kwa wazazi na jamii kwa ujumla..." asema Phillip Goff ambaye ni mwandishi wa makala hiyo... Profesa huyo akaongezea kwa kusema "utafiti wetu umegundua kuwa vijana wenye asili ya Afrika hawachukuliwi kama wanavyo chukuliwa vijana wazungu" na kufanya polisi kutumia nguvu na pia mbwa wanapoenda kuwakamata vijana kwani ni wenye vurugu kuliko....


Utafiti huo umewapitia kuwahoji polisi zaid ya 176 wengi woa wakiwa ni weupe "wazungu" na hilo ni usibitisho kuwa watu wenye asili ya Afrika kutoaminiwa na sheria au serikari pia na kuchunguzwa kwa karibu zaidi wanapo taka kujiunga na jeshi la polisi... utafiti huo umegundua pia 88% za vijana walio kamatwa na polisi ni wale wenye asili ya Afrika na walatino katika kipindi kifupi tu.

Saturday, March 15, 2014

LIL WAYNE ACHUKIZWA NA KANYE KWA SABABU YA ALBAM YA TYGA.


      LIL WAYNE ACHUKIZWA NA KANYE KWA SABABU YA ALBAM YA TYGA.
 Nyota wa muziki wa HIP HOP nchini Marekani Lil Wayne na pia
muanzilishi na mmiliki wa kundi la "young money" amechukizwa na kitendo cha
mwanamuziki wa kufoka Kanye west kuandaa(produce) albam ya mwanachama wa
kundi la young money Tyga...

Lil Wayne
"Kwanini Tyga hakunipa taarifa kabla ya kukubaliana na Kanye!?" ni swali
analojiuliza Lil wayne akiwa kama mmiliki wa kundi alilopo Tyga... Tyga
mwenyewe anasema kuwa "kila nilipokuwa nakutana na Kanye West kwenye
starehe au popote ni kama tuna uunganiko fulani hiv.." na hapo ndipo hamu
ya Kanye west na Tyga kupata nafasi ya kujadili kufanya albam ya "GOLD".

Kanye West
 Lakini mwisho wa siku Lil wayne afunguka na kusema "hapana bwana kijana
anapambana kwaiyo tumuache afanye anachoona ni sawa" kwa kusema hivo
inaonyesha kuwa Rapper huyo kukubaliana jambo hilo kiroho safi japo
hakupewa taarifa kabla... kaa mkao wa kula kwani albamu ya GOLD njiani.

Tyga

 
Blogger Templates